30 OKTOBA 2024
Manage episode 447731336 series 2027789
Contenuto fornito da UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations. Tutti i contenuti dei podcast, inclusi episodi, grafica e descrizioni dei podcast, vengono caricati e forniti direttamente da UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations o dal partner della piattaforma podcast. Se ritieni che qualcuno stia utilizzando la tua opera protetta da copyright senza la tua autorizzazione, puoi seguire la procedura descritta qui https://it.player.fm/legal.
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akimulika masuala ya amani na usalama hususan Gaza; afya ya ubongo kwa wanamichezo; biashara ya ndizi kaukau huko India na dansi na kujitambua huko Trinidad na Tobago.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini amemwandikia barua Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kusaka mshikamano na nchi wanachama baada ya Bunge la Israeli Jumatatu hii kupitisha miswada ya kusitisha shughuli za shirika hilo. Flora Nducha na maelezo zaidi.. Hoja ya ubongo kutikisika (concussion) wakati wa michezo imeibuka katika siku za karibuni na kulazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) kuingilia kati ili kudadavua kwa kina. Akiwa uwanjani akitazama mpira wa Daktari Tarun Dua, Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Ubongo WHO, anaeleza kwa muhtasari kuhusu tatizo hilo kupitia taarifa ya Cecily Kariuki.Katika makala, Assumpta Massoi anakupeleka barani Asia, kusikia jinsi wazo la biashara kutoka familia moja lilivyoleta nuru kwa kaya zaidi ya 20.Mashinani tunamulika jinsi dansi kulivyomweka huru mtoto mkimbizi kutoka Venezuela huko nchini Trinidad na Tobago.
…
continue reading
100 episodi